
Siku Nilalala Ndani by Keith Ang’ana

The Editors
Contributor
Published in Qwani 01
-
So hamskii, day flani around March, nilikuwa nimeenda kudishi lunch uko UoN sides za Klabu. Sa time natoka, si nkaamua kuteremka ivi University Way ndo niingie Tao. Kufika iyo roundabout ya Uhuru Highway na University Way, nkacheki karao akihanda msee wa nduthi. Mimi nani! Si nkaamua kutoa tenje niwapige mbota ndo niweke Twitter.
Sa ni ile nimegeuka nkaanza kutembea polepole ju naandika ma sentence apo kwa iyo picha. Kidogo kidogo naskia msee kando yangu ananishow “Kichana, epu leta iyo simu yako!” Nkashangaa rada yani karao ashanifikia? Nkafikiria anadai kumake call na simu yangu. So nkasema apana. Akaniangalia kidogo alafu akanishow, “My fren, ntapasua iyo kichwa yako na ii fimbo. Nakuambia mara ya mwisho, leta iyo simu.” So si nkamjenga tu simu. Jamaa akaenda straight mpaka gallery. Kumbe uyo karao alikuwa amenicheki nikimrecord hahaha. Akapigia some female police akamshow akuje apo.
Mi najuanga, ukisha involve karao mama, iyo itakuwa ngori kubwa. Makarao mamathe huwa na utiaji mob. So si uyo karao akamuok, uyu karao wangu akamshow, “Epu ona kazi yenye uyu kichana anafanya. Ananipiga picha nikishika mtu. Si yeye ni mtu wa media? Wametuzoea sana awa watu. Epu peleka yeye ndani!” Nkatry kuwashow mimi si msee wa media bana mi ni stude tu. Haha wao ni nani. Unadhani waliniskiza? So si uyo karao akapea uyo masa simu yangu alafu akaishia. Uyo masa akasema tuende ivo adi Central Police, ju ilikuwa tu apo mbele.
Sa tukitembea ivo, nkafikiria “Ama nitoroke?” ju uyo karao hakuwa na mbio. Lakini nkaona akona bunde, so nkaeza try ufala atanipiga tu risasi alafu story yangu iishe hivo. Sunajua tu masanse wa Kenya venye waukuwa. Lakini hata hivo, nlikumbuka akona simu yangu, na ni simu fiti. So singeafford kutoroka niache simu nyuma manze. Ingekuwa kaduda hata ningemwachia na rwabe ju nimshow ajibambe nayo. Sa ju ya hiyo story, nkaona acha tu niende na yeye polis steshen, ntajitetea tukifika uko ndani.
Sisi hao tukafika Central Police. Nimekuwa UoN miaka kumi (ukiongeza za strike), lakini sijai ingia uko ndani. Ii ndo ilikuwa first time. Si tukaenda apo penye makarao huandika report, nkaambiwa niketi chini na nitoe kiatu moja na belt pia, niziseti apo chini ya meza. Io masaa tu, jamaa flani mchafu akaingizwa ndani akarushwa apo kando yangu. Akalala chini kama ameinua t-shirt yake, nikacheki tumbo yake inahang ni kama ni izi pouch za ma kangaroo za kubeba watoi. Ao masanse wenye walimleta wakaanza kushout venye wamemkimbiza kutoka Khoja mpaka Globe ndo finally wakamshika. Jamaa saiyo anapumua tu apo chini ni kama anaenda kukufa haha. Hata hawakumwandikisha kitu. Walifungua tu mlango ya kwenda cell wakamrusha ndani ni kama ni regular.
Mi na uyo masa tukachill tu apo adi ule karao alinishika akarudi. Wakaanza kuongea nikiwa apo. Uyo mbuda akasema ati, “Hakuna hacha turushe uyu ndani. Venye amevaa, anakaa kuwa na pesa, so epu tumnyonye. Pea yeye simu apigie mamake amwambie atume ten thousand ndo atoke.” Heeeeeeh! Mi kuskia 10k nikasema haiwezi! Masangu atoe kapa kinde ju tu nlikuwa narecord sanse? Nkasema wakiskia, “Ah hapo heri tu nilale ndani.” Uyo karao mbuda akaboeka akasema “Haiya pasi, kucha tuandikishe OP”.
Nkamfuata tukaenda room ingine. Wakaandika jinangu, alafu apo kwa charges, uyo msee akachachisha bana aliandika “Incitement of violence & Obstruction of Police Duty.” Wah nikashangaa hizi vitu zote nlifanya saa ngapi? Alafu sa akasema watabaki na simu yangu ndo watumie kama exhibit. Nikakuwa handed over to karao mwingine sasa nikapelekwa cell manze hahaha.
Kulikuwa na corridor refu na rooms mob lakini sa nkaingia ya pili on my right. Eh hapo ivo nikapata watu ka kumi wamelala bana na ni lunchtime. Venye tu nliingia, jamaa flani wa nduthi akaamka. Akaanza kuniuliza maswali mob ati ooh uko shule gani ooh umefanya nini ooh unajua time yangu Babu Owino sijui alifanya nini. Eh nliboeka na uyo morio bana nan do nmeingia tu. Nkiwa tu apo story, jamaa mwingine akona uso ya odi akakam kando yangu alafu akasema “Eh bro si tulale”. Bila hata kufikiria, si pia mimi nikaingia doz (Time nachapiana ii story uku nje, ndo msee aliniuliza ati what if uyo morio alikuwa anadai kunidishi Sim 2 kama watu wa Inda, na mi nlikuwa naitikia tu? Eh enyewe nkasema heri hivo hakuwa na intentions mbaya). Unajua uko ndani hakuna shiet ya kufanya, sa ndo upitishe time, inabidi udoz tu. Nlikuwa nmedungia floral shirt ya white, na ki khaki trouser smart ya black, lakini nkasema ka mbaya mbaya, acha tu nilale nizichafue.
Unajua huko cell hakuna saa na hakuna dirisha, lakini kuna openings tudogo huko juu karibu na ceiling. So the only way kujua time, ni kuangalia venye jua inachapa io ukuta on the opposite side. Time nliingia cell, ilikuwa 2:30, sa nkamaster venye iyo rays za jua zinachapa iyo wall. Time naamka, nkaona bado rays za jua ziko same. Nkasema fuck! Nisikuwe nimelala 20 minutes pekee na venye naskia nimemaliza usingizi yote mpaka ya next year. Ndo kugeuka nyuma yangu (ama labda alinidishi Sim 2. Enyewe alikuwa anafanya nini nyuma yangu), nkapata ule odi hayuko. Alikuwa anatembea tembea tu. Nkamwuliza ni saa ngapi akasema 5:30. Heh, sema kufurahi at least time imesonga sa siku inaenda kuisha. So nkaamua kuketi nkimedi.
After kedo 30 minutes, msee akapita nje ya mlango akitushow ati ni githaa ya supper. Eh, tunakula supper 6:00, kwani ni high school? Lakini enyewe watu husema shule ni jela, so sasa nkaona it makes sense. Tulitoka kwa our individual cells tukapanga line apo kwa corridor, msee mmoja ndo alikuwa anaserve food kutoka kwa ndoo uko mbele. Sasa hamskii supper, unapewa container kama ile ya Blue Band, alafu unaserviwa vijiko mbili za githeri, alafu ni hivo. Hiyo sasa ndo supper. Hakuna hata kijiko ya kukulia. Unakunywa izo mahindi na maharagwe ni kama ni juwis. Mi nakushow wasee wengine walimaliza food yao in 2 minutes, mi saiyo nang’ang’ana na yangu kama kitu ingine. After 30 minutes bado sikuwa nimemada, ndo ule odi akaniuliza, “Eh na unateseka” nkamshow “Manze sijazoea kukula ivi” akanishow “Hi indo maisha ya mwanaume sasa”. Ule msee wa nduthi mwenye nli ignore mwanzo akakam akanishow ati nsimalize food yangu, ju katikati ya usiku naeza skia njaa, so nitaihitaji. Si nikafuata advice yake nikaweka iyo githeri penye nlikuwa nmedoz, ju iyo sasa ndo ilikuwa spot yangu mpya.
Io masaa ilikuwa around 6:30. Kila mtu mwenye alikuwa amedoz mchana alikuwa awake, so watu tu walikuwa wanapiga story everywhere. Nikaamua sasa ii ndo chance nikuwe Henry Morton Stanley, nipige exploration ya cells zote. So si nikatembea kutoka ya kwanza, yenye ilikuwa imeandikwa “JUVENILES” apo kwa mlango, lakini sa ndani hakukuwa na watoi. Ilikuwa rende flani ya ma bazuu walikuwa hadi na ma blanketi na fegi wanavuta. NI kama io ndo ilikuwa baze ya ma dip stet wa cell. Venye nliingia tu ivi, ule mwizi alikuwa ameshikwa the same time na mimi akaniona alafu akaniuliza, “Eh brathe ukona ndovu?” Nikasema zae. Akanishow ni ju ya venye lips zangu zinakaa nikama nimeseti chavez (enyewe ukicheki chini ya my lower lip huwa imefura ni kama nimeseti chavez hahahah). Akageuka akachapia ao ma inmates wengine venye nlishikwa ju ya upuzi, na venye nlikuwa nmenyenyekea tukiwa apo nje na makarao. Let me tell you Maina, hakuna kitu ya upuzi ka kuonewa huruma na ma odi. Wako apo wanakushow “Ah izea bazenga. Ao makarao ni mazimbiting. Tutawacane tukitoka apa. We usikai tense morio. Ebu jisaidie kishash apa ivi.” Alafu wanakugotea na ngumi mbwegze. Yaani izo majina wanatumia hadi hazikuconsole. Zinafanya adi uskie ni ka unaibiwa.
Anyway, nlitoka apo nkaenda cell ya pili. Io ilikuwa imeandikwa “WOMEN”. Kwa zote, hii ndo ilikuwa na the most protection. Ilikuwa na grills tatu, na bado imefungwa na padlock. Though nkichungulia ndani hakukuwa na msee. So nkaachana nayo. Ya tatu, ilikuwa imefungwa na ndani, na nlikuwa naskia masauti. Sijui kiherehere gani iliniambia nichungulie na kashimo apo chini. Kufanya hivo, nkacheki light kama ya simu. Kumbe ii ndo ilikuwa keja ingine ya dip stet. Awa wasee walikuwa na tenje, na ni kama nlikuwa na make calls. Noma. Enyewe adi mimi kama simu yangu haingekuwa evidence, labda ningeweza kuingia nayo. Ju hawa makarao hawakunipiga search nikiingia cell. Waliniambia tu nitoe vitu niko nazo kwa mfuko niweke kwa drawer. Si nikatoa tu kifunguo ya nyumba (u itanisumbua nikilala) lakini nikabaki na fare ya kwenda home (coins za 30 bob). Ah nikaachana na ao wasee. But at least sasa nilikuwa nimejua where to go in case ntahitaji kucall.
Cell ya nne ilikuwa ile yangu sasa. Kulikuwa na zingine nne, zote za wanaume. So in short, kulikuwa na cell moja ya watoi, moja ya madem, na sita za mandume. Eh hio ratio ni weird. Kumbe siushikwa wengi ivo. Alafu sa si nikafika uko mwisho ya corridor. Kulikuwa na tap penye ule odi flani beshte yangu alikuwa anachota maji. Hata si tap, ni pipe imeburst tu hahaha. Maji ilikuwa tu inamwagika chini alafu ndo kuangalia, nkagundua inaenda tu kwa choo.
Choo nayo heh wacha tu! Kumbuka tulitoa kiatu tukiingia cell, sindio? So sasa kwa choo, maji imeflood adi ankle length. Kuna urinal, na latrine mbili, lakini zote ziko nauko mwisho. So ndo ufike hapo, unafaa kuruka ruka na mguu moja kama ile game ya primary ya wasichana yenye wanachora boxes chini na chalk alafu wanaruka ndani ya izo boxes. Sa ukishafika kwa latrine, unafanya biashara yako ka umesimama na mguu moja kama flamingo, alafu unatoka. Mi kitu tu ilikuwa inanishangaza, ni sasa the women watatumiaje izo choo. Ju huwezi squat na mguu moja ki-Bruce Lee hahaha. Na usisahau choo zimejaa mavi. Ulidhani zinaeza kuwa safi kuliko zile za kanjo? Wapi joh! Hizi hata hazina mtu wa kuziosha.
So by the time nimemaliza kupiga tour ya cell, ni kama saa moja usiku ilikuwa imefika. Nikama io masaa huwa prime time; si ya news pekee, lakini pia ya kurusha watu ndani. Heh watu walikuwa wanarushwa ndani ka venye mtu hurusha njugu kwa mdomo. Sa si nikaamua kuenda kusimama apo kwa mlango ya cell. Si unajua venye ka Form 2 ama Form 4 husimama kwa mlango ya dorm ma form 1 waki admittiwa, ndo ajue ule mwenye atabully virahisi? Baas hvo ndo nlikuwa nmesimama apo. Kukaa kwa cell 5 hours si jokes. Nlikuwa nshakuwa experienced so nlikuwa najiona ki-form 2.
Watu most wenye walikuwa wanaingizwa ni wababa wazee, so sikuwa na haja nao. Ni ile tu walikuwa wanalia ooh wameshikwa ju ya reasons za upuzi nini nini. Lakini ka mi mwenyewe ni mtoi na sicomplain, wewe ni nani na izo ndevu zote na fudhi?
So ile kubangaiza ivo, nkacheki kaboy flani kameingizwa. Alikuwa amevaa tu ka mimi, floral shirt na trouser, so nikajua haka ni ka rich-kid. Si nikasema ah baaas at least nimepata arif for the night. Nikaishia ivo nikamgotea. Eh jamaa anabonga kilami bana. Nkajipiga intro alafu nikamuuliza, “Worrayuduin in here fam?” Akanishow venye sijui ye ni worker wa msee flani anaendea Governor apa Kanairo, lakini sa amekataa kuchukua bribe so uyo mkubwa amesema arushwe ndani. Eh mi kuskia gavana nikasema wah kumbe msee anaeza pata connections kwa cell hahaha ebu ni stick by his side. Si nikampelekwa kwa my State House pale cell number 4 nikamshow apa ndo miuchill. Akasema ‘Cool”.
Nkidhani ilikuwa imefika 7:30, ju sisi wote tuliitwa apo nje kwa ki open area tukakalishwa chini wakapiga roll call ya kila msee wameshika io day, alafu tu mnarudi cell. Ule msee wa nduthi aliona niki shiva shiva akanijenga kabuti moja, ju sa alikuwa na nne. Alafu akanishow usiku kunakuwanga kubaya uku, so nikiweza nipigie mamangu akuje anitoe. Mi saiyo nlikuwa nataka tu kulala ndani, niskie venye inafeel, ju inakuwanga kwa bucket list yangu. Kawaida miusema wewe si mwanaume kama hujai lala ndani. Huwezi nishow shit. So nlikuwa nimepanga ninyamaze tu penye niko, nisipigie mtu simu, washangae penye niko, alafu sa the next day nipelekwe court, nilipe fine ya either 500 bob ama thao, alafu niachiliwe niende nipige appearance home kama Yesu after resurrection.
Anyway after roll call tukarudi cell. Si sasa wale wasee walikuwa wamedoz mchana walikuwa wamechangamka, plus sasa ule mwizi nliingizwa cell at the same time nayeye. Kumbe ao wote ni ma wezi wa simu hapa Tao. Walikuwa wanatushow mastingo zao bana. Mmoja anasema venye anatembeanga na beshte yake kwa jam OTC alafu wanatafuta magari personal, beshte yake anapita side ya passenger anagonga side mirror inasonga. Sasa ye anagongea dere dirisha anamshow acheki ile side mirror venye inakaa. Dere kugeuka, yeye anaingiza mkono kwa dirisha anaiba simu anahepa. Hii ni a very old trick in the books. Akatushow sasa venye leo aliibia mdem simu kwa mat, conductor akamwona, akaita wengine haraka wakamkimbiza kutoka OTC mpaka Tea Room, wakamshika apo alafu wakampeana kwa sanse.
Ule mwenye nliingia na yeye sasa aka take center stage. Akatushow venye sa leo alikuwa apo Khoja, akacheki msee akitumia simu kwa mat. So akaizunguka na nyuma, alafu akaenda kwa iyo dirisha ya uyo msee, akaipiga na design flani ikafunguka, alafu akachukua iyo simu haraka before ata mwenyewe arealise. Sa after kuchukua, si donda pia alikuwa amemcheki, na karao wa apo Khoja, wakaanza kumfuata. Mwizi sa akaenda iyo sidewalk ya Old Nation House alafu akashout “Kanjo! Kanjo!” akikimbia pia. Hao ma hawker wote wa Tom Mboya Street kuskia ivo, wote wakafunga mizigo zao wakaanza kukimbia na yeye. So ni ile amepotea katikati yao, hadi haonekani sasa. Wakakimbia ivo adi Globe Roundabout. Apo sasa ndo wakarealise kumbe akuna kanjo nyuma yao, plus uu msee mwenye anafanya wakimbie, hana mzigo, so ata si hawker. Ndo konda akatokea nyuma yao akashout ati uyo ni mwizi. Si sa hawkers wakamgeuzia wakamkimbiza mpaka Nairobi River, akadive ndani. Mmoja akarusha mawe ikamgonga kisogo, ndo sa by the time anaswim mpaka io side ingine, karao alikuwa ashafika. Hivo ndo akarushwa ndani. Sasa ata iyo simu alikuwa ameiba ilikufa. Na pia akatuonyesha fegi alikuwa nayo kwa mfuko imekuwa wet. Najua inakaa kuwa story ya jaba lakini hamskii ni ukweli.
Tena ao wezi wawili sasa wakaanza kuongelelea time wamerushwa ndani uko Kamukunji (based on story zao, hawa wasee ni kama wamelala ndani kila pahali ata Lodwar). Sasa ju hawananga familia ya kuwa bail out, wao hufanyishwa community service alafu ndo wanaachilia. So io siku, uyo mwizi main alikuwa ameambiwa aoshe io main room ya kureport. Hakukuwa na karao apo at the time. Sijui walikuwa wapi. So ni ile anafagia fagia, alafu kiasi kiais akafungua drawer, akapata simu ya kila mtu mwenye amerushwa ndani iko hapo. Waah sema morio kunice mbaya. Aliweka tu kifagio kando, akaanza kuweka izo simu zote kwa waist. Akavaa ka simu 15 kwa waist kama belt, alafu akawalk out. Unajua ni ile anatoka kwa room ya mapolisi, sio cell, so hakuna mtu alimshuku. Eh venye alifika apo nje alitoka keuti akaenda akauza izo simu zote.
Anyway, ao wasee wakaendelea ivo ku exchange stories ivo tu, mpaka at the end nikaogopa CBD. Yaani kama watu wakona ma tactics ivi, si basi heri nisiwai toa simu nikiingia tao. Kama unataka kunipigia ni ungoje mpaka nitoke Tao ama niingie kwa building. Otherwise awa wezi wanaeza ingia mpaka kwa socks yako kama umeficha simu hapo. All the while, uyu rich kid beshte yangu alikuwa ananipigia story na kizungu. Sa ni ile anachoma, ju eh awa wezi wakiskia tunabonga ivi si watajua sisi wote ni marichkid wapange venye watatutoka kila kitu adi kidney. Nikasema apa siezi kaa na uyu richkid mpaka usiku. Lazima nitafute venye nitamhepa.
So kitu 8:30 tukaitwa tena pale nje sisi wote. This time sasa ilikuwa OCS ndo ako hapo. Ulikuwa unatajwa jina, unasomewa mashtaka, alafu unaambiwa kama utapelekwa court the next day ama utaendelea kulala ndani. Ikafika changu, akasoma jina na charges, alafu nikainua mkono. Akaniona na iyo kabuti kubwa akauliza, “Haiya ni wewe ndo unasumbua mapolisi hapa sindio? Na wewe ni wa sacco gani?” Nikatry kusema mi si mtu wa nduthi, but before hata nifungue mdomo, akashout, “Nyamaza!” alafu akasema iyo utaenda kuelezea watu wa korti kesho. Nikasema wah, thingz are gerrring real. Ule richkid akatajwa, alafu mashtaka yake ilikuwa something big, kizungu mingi adi sikuelewa, mpaka kila mtu akashangaa tu si apelekwe tu ICC mara moja. Mi kuona ivo nkasema sitaki ku associate na uu criminal mkubwa ivi acha ntamhepa tukirudi cell. By that time pia, kulikuwa na wamama wawili wameletwa, na walikuwa wamekaa nyuma ya OCS, ju of cos hawangekaa na sisi mandume. Time walitajwa, kila mtu ali whistle na kusherekea ni kama wamepita exam haha. Enyewe nikaona kumbe cell za madem ziko under lock and key ju niggaz in here are too horny. Otherwise ingekuwa open, sisi wote tungeingia uko in the middle of the night tupige train wazimu kuliko SGR.
So after that tukaambiwa turudi cell. Nikakumbuka ile cell ya simu, kumbe uu msee wa nduthi alikuwa huko pia. Nkamuuliza ka naeza kam akasema sawa. Somehow nlikua convinced nisilale ndani. Ju every now and then mtu alikuwa anatolewa, mpaka nyi wenye mnabaki mnafeel ni kama hamna watu wanawajali. Ilikuwa inafeel kama wazazi wako wasipokam visiting. Wengine wameketi wakikula food na we saio uko tu dorm umelala hahaha. So si tukirudi cell nikaingia io. Tulikuwa wanne tu. Mimi, nduthi guy, phone guy, na some mid-twenties guy. So si tuka take turns kumake phonecalls, me being the last ju mi ndo nlikuwa nmeingia wa mwisho.
Kuchukua simu, nikacall masangu. Nlikuwa naogopa asichukue ju ni unknown number. So venye alishika, nkakuwa straight to the point, “MUM! Ni Keith. Kuja unitoe Central Police”. Hmmmmmmmmmm. Wacha mamangu askie Central Police. Wacha aanze kunipiga lecture. Ati ooh “kijana wangu, nimekusomesha vizuri, nikakulipia school fees yote, nikakupea kila kitu unataka kwa nyumba, alafu ushaanza kushikwa na mapolisi? Unajua venye io ni mbaya?” Sa niko apo nafikiria like, mum first of all napiga simu illegally, unawaste credo ya mwenye simu. Izi ni vitu unaeza niambia in person. So after amenilecture 3 minutes nikamkatiza nikamshow, “Ebu we kuja” alafu nikakata simu.
30 minutes passed. 45 minutes. 1 hour. Askari anakam akitoa watu wengine lakini mimi haniiti? Nikashangaa rieng? So nikaomba uyo msee tenje tena nikadungia masangu nangos kumuuliza rada. Akanishow ati OCS amemshow ati niliita wasee wa nduthi nikawa chachishia ati tuende tupige makarao. So ju ya hiyo story, siwezi achiliwa. Mimi ni a criminal of the state. Hiyo saa mamangu anaongea ni kama anataka kulia. Saiyo mi nko apo nashangaa tu lmaoooooo nimefanya izi vitu zote saa ngapi? Si OCS aangalie ata venye natoshana before adanganye. Anyway, niliona sasa fate yangu ime sealiwa. So acha nidoz ningoje kesho.
Si tulikuwa wanne io room, so nkaenda corner moja, nikajiseti doz. Amerix husema kudoz kwa floor once a month ni fiti, ju inastretch spine yako, so nikasema acha leo nitry out hio medication yake. Unajua uzuri miupata usingizi within 2 minutes after kujiekelea, so hata hapo usingizi ilikam bila stress. Nakumbuka tu kitu around 11, mlango ilifunguliwa alafu watu wengine ka 20 wakarushwa ndani. Nliskia tu ma movement alafu nikaendelea kulala. Tena pia in the middle of the night, nlikuwa nageuka from one side to the other, alafu ile 30 bob ilikuwa kwa mfuko yangu ikaanguka. Wacha kila mtu kwa cell aamke! Eh ilikuwa inakaa ni kama watanivamia . . . ju ya 30 bob! Anyway, msee ako kando yangu alini whisperia nirudishe izo coins kwa mfuko haraka, alafu nikarudi doz.
The next thing nakumbuka ni karao akitembea kwa corridor akishout “Keith Angana! Keith Angana!”. Nikaamka nikakimbia kwa grill ya cell nkasema “Ni mimi! Ni mimi!” Eh akakuja akanifungulia mlango, tukaanza kutembea nay eye. Ilikuwa imefika asubuhi , ju nlikuwa naona jua nje. So tukatoka io baze ya cells, nikapatana face-to-face na OCS hapo nje. Akaniuliza, “Unajua uyu mtu?” alafu akapoint in the direction opposite him. Mamangu akatokea apo nyuma ya karao dramatically, ni kama ana act Drama Festival hahaha. Nikasema eeh namjua, ni mokoro wangu. Akaanza kusema venye nimemtesa, anga alikuja cell jana usiku late na akarudi mkono tupu anga nimefanya hajalala usiku nzima, mara tena nimefanya ameamkia cell. Nikaambiwa niseme pole. Ilikuwa inakaa ni kama niko staffroom alafu nateteshwa ju ya grades hahaha. Anyway, karao akauliza mokoro wangu, “Na uu kijana wako unaona venye izi nywele zimesimama? SI tuziteremshe na makasi?” Masangu akasmile akasema “Hapana. Wacha tu ntampea pesa aende kinyozi.” Alafu OCS akasema “Sawa unaeza enda na kijana wako.”
Apparently ilikuwa time ya chai na dibre, sa nlifeel vibaya nlihata breakfast ya police station. Otherwise ningei piga review niwasho ka iko fiti ama iko njei. Nikakumbuka tena nikona jacko ya ule msee wa nduthi, na huskii sikuwa najua jinake, so nkaiacha tu apo kwa counter nikasema akitoka atajua ni yake. Aaaah hata sikumshow Asante ne venye alikuwa ameniokolea usiku. Sa si nikakimbilia simu yangu bana nisipate imeibiwa na ule mwizi hahaha. Kucheck time, ilikuwa 6:58. Simu yangu ilikuwa imebakisha 2 minutes alarm ianze kulia, na venye inakuwanga loud. Kama ingebaki hapo ianze kulia, ao makarao wangeudhika waivunje ama waitupe nje. Anyway, nilipata pia missed calls from my woman, but do I say? Ofc pia yeye alikuwa worried about my whereabouts. Ebu tafuteni mtu anawajali hivo.
Sa after kuchukua vitu zangu na kiatu, si nikatoka sasa na mamangu kuenda kwa gari. Hakutaka kuniongelesha so alitembea mbele nikamfuata nyuma. Gari ilikuwa ime parkiwa mbali, so io long walk to freedom (kama Nelson Mandela akitoka Robben Island) ilikuwa weird. Time tunafika kwa gari nikatry kufungua mlango ya mbele akasema, “Apana. Kaa uko nyuma. SItaki kukuona!”. Nikachorea tu haha. Sa si tukianza kusonga akaendelea kunitetesha tetesha apo, lakini mi nlikuwa nafeel fiti at least nimetick off kulala ndani kwa bucket list yangu. Ilikuwa kama kutahiriwa mara ya pili. Inakufanya ukuwe ndume Zaidi.
Anyway, my mom alinisindikiza mpaka stage, alafu akanipea fare na pesa ya kunyolewa, akasema io nywele lazima iteremke (nlikuwa na Afro safi sana io time). So si nikaenda mtaa nikapiga ngasha fresh alafu nikapiga cut. Nikacall my dad nikamchapia io story. Aliisha mbaya, ju pia yeye some years back alikuwa amebambwa na masanse akarushwa kwa mariamu akalala ndani, alafu mamangu akaishia akamtoa kama amejam. Nkamshow venye mum pia alikuwa amejam akinitoa, tukacheka iyo story.
Hiyo sasa ndo story yangu ya venye nlilala cell.
To communicate more with the writer, find him on:
Email: keithangana@gmail.com
-
Image by DJ Krowbar
Join the Conversation
(0 comments)Sign in to join the conversation
Share your thoughts and engage with our community

